Alikiba afunguka salam aliyompa Diamond

0
521

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kusema kuwa anashangaa watu kujadili aina ya salam ya mkono aliyompa mwanamuziki mwenzake, Diamond Platnumz katika msiba wa Agnes Masogange.

Alikiba amefunga hayo leo wakati wa mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv.

Alikiba amesema kuwa ile salam ni salam kama zilivyo salam nyingine hivyo kwake hakuona kama kuna tatizo kumpa mkono kwa kumgeuzia kiganja ila watu wanapenda kukuza maneno.

Alikiba aliendelea kusema kuwa watu wanapenda kukuza mambo mitandaoni kutokana na upinzani uliopo katika yake na Diamond kwenye muziki.

Ikumbukwe katika msiba wa Agnes Masogange Alikiba na Diamond walikutana katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam ambapo Diamond alimsalimia Alikiba na Kiba kumpa mkono kwa kumgeuzia kiganja jambo ambalo lilizua gumzo mtandaoni.

LEAVE A REPLY