Alikiba afunguka kuhusu sapoti kutoka kwa mama yake mzazi

0
1229

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘’Mvumo wa Radi’ Ali Kiba amefunguka na kumtaja mama yake mzazi kama mtu ambaye amekuwa akimsapoti kimuziki Kuliko Baba yake.

Ali Kiba amekuwa akionekana akiwa na ukaribu zaidi na mama yake Kuliko na Baba yake hata Kwenye mitandao ya kijamii amekuwa akionekana akiwa karibu na Mama yake.

Ali Kiba ameweka wazi kuwa Mama yake ndiye mtu aliyemsapoti katika mziki wake tangu anaanza Mpaka sasa tofauti na ilivyokuwa kwa Baba yake Mzee Salehe.

Ali Kiba alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo  kimoja cha habari ambapo amefunguka na kusema kuwa mama yake ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wake kuliko baba yake.

Katika jamii zetu za Afrika wazazi wengi wamekuwa wakiamini kuwa muziki au sanaa yoyote ile ni uhuni lakini baadhi ya wasanii kama Ali Kiba wamekuwa wakifuta dhana kutokana na kuwa kioo cha jamii bora na mfano wa kuigwa.

LEAVE A REPLY