Alikiba adhamiria kuwasadia wakimbizi Kigoma

0
28

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameanzisha kampeni ya kukusanya michango mbalimbali kwa ajili ya kupeleka kwa watu waishio kwenye kambi za wakimbizi Kigoma.

Alikiba amesema kuwa wadau mbalimbali watakusanya michango mbalimbali kwa ajili ya kupeleka kwa watu walio kwenye kambi za wakimbizi mkoani Kigoma.

Michango hiyo itajumuisha mavazi, vyakula visivyoharibika, mazao, magodoro, madawa ya binadamu au mchango wowote.

Alikiba na wasanii wengine watapokea michango hiyo ili kupeleka mkoani Kigoma kwa ajili ya kutoa misaada kwa wakimbizi hao wa mkoani Kigoma.

Alikiba anatarajia kufanya show mkoani Kigoma akisindikisha na baadhi ya wasanii wanzake wa Bongo Fleva ambapo wataongoza mkoani humo kwa ajili ya show hiyo.

LEAVE A REPLY