Alikiba adai hafanyi muziki kwa ajili ya tuzo

0
55

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa anapokuwa anafanya muziki kikubwa anaangalia zaidi kuwafurahisha mashabiki na sio kupata tuzo.

Kauli hiyo ya Ali Kiba imekuja siku moja baada ya taarifa za kwamba yeye pamoja na wasanii kama Diamond na Wengineo waliokuwa wanawania tuzo za Afrimma kukosa tuzo.

Kwa miaka miwili mfululizo Ali Kiba amekuwa akifanya vizuri katika tuzo za Afrimma ambapo hta mwaka jana alimbwaga Msanii mwenzake Diamond Platnumz na kuchukua tuzo.

Ali Kiba amefunguka na kusema hajaumizwa sana na kukosa tuzo kwani tangu Mwanzoni hakuwa alifanya ili kupata tuzo.

Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu kinachomuumiza kama akiona familia yake inakuwa inatukanwa Kwenye mitandao ya kijamii.

 

 

 

LEAVE A REPLY