Alikiba adai ategemei pesa za ‘views’ Youtube

0
126

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye sio miongoni mwa wasanii wanaotegemea kupata pesa kutoka katika ‘views’ za Youtube.

Kiba ametoa kauli hiyo baada ya video yake ‘Mvumo wa Radi’ kushindwa kufanya vizuri katika mtandao wa Youtube.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kuna mchezo anafanyiwa msanii huyo ili asiweze kufikisha views wengi kama ilivyokuwa kawaida yake kila atowapo video.

Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema “tunajua kwamba kuna hizi biashara za kuweka ma-robot katika ‘Youtube’ ili ionekane watu wana ‘view’ kwa wingi.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Mvumo wa Radi’ aliouachia wiki hiyo ambapo hadi sasa hivi una views milioni 1.3 katika mtandao wa youtube.

LEAVE A REPLY