Alikiba adai anahofia kufirisika akitoa nyimbo kila mara

0
689

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kusema kuwa anauwezo wa kutoa nyimbo kila siku lakini anahofia kufirisika kwakuwa muziki unatumia pesa nyingi.

Kauli hiyo ya Kiba inakuja baada ya mashabiki wake kujaji kwanini mwanamuziki huyo anakaa muda mrefu bila kuachia ninyimbo mpya.

Kiba amesema kuwa muziki ni biashara na kila biashara huwa na msimu wake kwa hiyo hatoweza kutoa nyimbo kila mara.

Pia amesema kuwa hadi muziki unamaliza mwaka masikioni mwa watu ni kwamba una miguu mirefu, yaani muziki wake unaishi lakini haimaanishi kuwa hana uwezo wa kutoa nyimbo kila wakati.

Alikiba kwa sasa anatamba na ngoma mpya ‘Mvumo wa Radi’, ambao unaendelea kufanya katika vituo mbali mbali vya radi na Tv nchini.

LEAVE A REPLY