Alikiba aanza mwaka kwa kishindo

0
20

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Alikiba ameuanza mwaka 2021 kwa kufanya kazi nyingi baada ya kuonekana katika kazi mbali mbali zikiwemo zake na za kushirikishwa.

Alikiba tayari ameonekana kwenye ngoma tatu tofauti ndani ya wiki tatu, ikumbukwe aliahidi kuwa sasa hivi atakuwa akitoa nyimbo mfululizo ili mashabiki wake wafurahie muziki mzuri.

Alikiba ameanza hivyo baada ya kushirikishwa ndani ya ngoma tatu mfululizo lakini pia akiahidi kuwa mwaka huu ataachia album yake katikati ya mwaka huu.

Alikiba ngoma yake binafsi ya mwisho ilikuwa ni MEDIOCRE ambayo aliiachi mwezi wa tisa lakini baada ya hapo sasa hivi amejitokeza katika ngoma tatu tofauti za kushirikishwa.

Alianza na ngoma ya DJ Sbu kutoka Afrika kusini katika ngoma  ya “Nakupenda” wiki mbili zilizopita na baada ya wiki moja tena alijitokeza kwenye ngoma ya Proud of you aliyoshirikishwa na Darassa lakini siku moja iliyopita ameshirikishwa na msanii kutoka kenya Otile Brown katika ngoma ya In love.

LEAVE A REPLY