AliKiba aanza kushoot Video ya “Aje remix” Afrika Kusini

0
466

Staa wa Bongo fleva, AliKiba ameanza kutengeneza video mpya ya wimbo “Aje remix” aliyomshirikisha msanii kutoka Nigeria, M.I baada ya kufanya vizuri na original version ya wimbo huo.

AliKiba ameweka kambi nchini Afrika Kusini kuandaa remix ya wimbo huo ambapo hatua za awali za video ishaanza na inakaribia kukamilika.

Kolabo hiyo ya ‘Aje’ akiwa na M.I ilivuja katika mitandao ya kijamii wakati haijamalizika hali ambayo ilimfanya AliKiba kuachia original version kwanza alafu baadaye kuachia remix hiyo.

Kutokana na video ya AliKiba iliyozagaa katika mitandao ya kijamii, ikimuonyesha mwanamuziki huyo akiwa location Afrika Kusini huku akizungumza project hiyo.

Staa huyo kwa sasa yupo Afrika Kusini akishoot video mbili mpaka sasa, moja ya kolabo yake na Barakah Da Prince na nyingine ya kolabo yake hiyo na M.I kutoka Nigeria.

LEAVE A REPLY