Alichosema Rama Dee kuhusu sakata la madawa ya kulevya

0
318

Mwanamuziki nyota wa RnB nchini, Rama Dee amesema kuwa aungi mkono kwa baadhi ya wasanii kuwekwa ndani kuhusu madawa ya kulevya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rama Dee ameandika.. “Mimi kama msanii, Siungi mkono wasanii kuwekwa ndani Ila ninge muunga mkono Kama angeweza kuziba mirija ya Wauzaji Papa kuwafikia wasanii na watanzania kwa ujumla!

Toka nipo mdogo wauza unga wanafahamika na majina yao yapo kwenye mitandandao lakini sijawahi ona wakikamatwa wala kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari! Hata hao polisi pia sijaona picha zao!”

Ameongeza, “Wasanii ni watu Kama watu wengine tu… so unapo anza kuaribu biashara zao kwa sababu tu upo na power ya uwongozi sidhani kama ni busara!

Ushauri wangu kaa na viongozi wenzio ambao walikutangulia kwenye uwongozi uliza why walishindwa then anzia hapo! Unajuwa haya mambo unaweza ona ya kawaida Ila yanaweza kuharibu maisha ya watu kuliko hata huwo Unga! Haswa wasanii.

Namuunga mkono Nape kuwa kuna njia za kutumia ambazo zinalinda sheria ya mtuhumiwa! Ila ukitumia nguvu bila Akili ni sehemu mojawapo ya kuwapatia pesa Wanasheria bila msingi wowote! Kukamata watu kwa kuhisi ni utaratibu mbaya sana! Kumbuka kuna watu wapo na chuki za maendeleo ya watu wengine.Unaweza ukasikia hata Tale anauza unga ambae ni rafiki yako, sijuwi utafanyaje hapo.

Mimi naona plan yako imeanzia sehemu si sahihi rudi nyuma Anza tena ni hayo tu, halafu hakuna movement nzuri Kama movement ya kutumia power ya wasaniii na jamii kiujumla. Fanya kazi yako Mh. makonda waache wasanii watafute mkate wao wa kila siku! Rama Dee!”.

LEAVE A REPLY