Alichosema Irene Uwoya kuhusu Dogo Janja

0
780

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa bado hajaona mwanamke ambaye anaweza kimpindua kwa mume wake staa wa Bongo fleva Abdul Chende ‘Dogo Janja’.

Uwoya ameweka wazi kuwa yeye ni mwanamke anayejiamini sana na anaamini kuwa mume wake anampenda na anajua kuwa hakuna mwanamke anayeweza kuingilia penzi lao.

Irene Uwoya amesema alipoamua kuingia kwenye ndoa na mwanamuz­iki huyo alijua wazi ‘nyakun­yaku’ wapo, la­kini kikubwa anajiamini.

Uwoya amesisitiza kuwa hata mume wake aende wapi na aone mwanamke gani hawezi kumuacha yeye maaana anajiamini na anaamini kuwa amekamilika idara zote.

Uwoya na Dogo Janja walioana mwaka jana ambapo wiki iliyopita walifikisha miezi Tisa katika ndoa pamoja hiyo.

LEAVE A REPLY