Alichosema Dogo Janja kuhusu Irene Uwoja

0
115

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema kuwa anafurahishwa na jinsi Irene Uwoya anavyopambana lakini anatamani kuona akifanya vitu tofauti na wengine.

Dogo Janja ameongelea vitu anavyovikosa kwa Irene baada ya wawili hao kutengana na kusema kuwa ana-miss kumpiga makofi na amefunguka na kuweka wazi kuwa kuna vitu ambavyo wameshafanya pamoja.

Mwanamuziki huyo amefunguka hayo wakati wa kutambulisha ngoma yake mpya ya ‘Yente’ na aliongeza na kusema anafurahishwa na jinsi Irene Uwoya anavyopambana lakini anatamani kuona akifanya vitu tofauti na wengine.

Amesema kuwa “Namiss kumpiga makofi ,Kuna vitu vingi ambavyo tumefanya pamoja na Irene Uwoya moment ni nyingi kikubwa namiss kumpiga makofi, nafurahi kuona jinsi anavyopambana na toka zamani nilikuwa natamani kuona akifanya vitu vyake na kumtofautisha na watu wengine”.

Wawili hao kwasasa wameachana na kila mmoja ameanzisha mahusiano mengine ambapo Dogo Janja kwasasa ameanzisha mahusiano na mwanamke mwingine kutoka jijini Arusha.

LEAVE A REPLY