Alichoposti Harmonize kuhusu Rich Mavoko

0
167

Mwanamuziki wa  Bongo Fleva, Harmonize ameandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Instagram, kuhusu ukimya wa msanii mwenzake Rich Mavoko.

Sasa kupitia ujumbe huo ambao ameuandika Harmonize unaeleza kuwa  “Familia ngapi zipo nyuma ya Rich Mavoko na zinamtegemea yeye kwa kila jambo, hasa hili la kupata mkate wa kila siku.

Vipi kuhusu ndoto za familia hizo na zinaishije kwa wakati huu, ndoto ngapi za wasanii ambao wanategemea kuzifikia hizo ndoto kupitia Mavoko”.

“Mungu ana sababu na maana yake kaka, kama mdogo wako nakuombea, najua ukimya wako una maana kubwa sana ndani yako, ninachojua ni kujiweka sawa na kutuletea kazi zingine, tunakupenda na tunakuombea mungu akufanyie wepesi, mdogo wako rafiki yako nipo hapa muda wowote, Ramadhan Kareem”.

Mara ya mwisho kwa Rich Mavoko kupost picha kwenye akunti yake ya Instagram, ilikuwa ni Januari 1,2020, katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya, pia ikumbukwe wawili hao wameshafanya kazi ya pamoja mwaka 2017 kwenye wimbo wa “Show Me”.

 

 

 

LEAVE A REPLY