Alichopost Afande Sele kuhusu Makonda kuvamia Clouds Media

0
375

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Afande Sele kupitia ukurasa wake Facebook ameandika ujumbe kuhusu tuhuma za mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuvamia studo za Clouds Media siku ya Ijumaa.

Kupitia Ukurasa wake wa Facebook, Afande Sele amelezea hisia zake kufuatia tiko hilo ambalo limekiki sana mwishoni mwa wiki.

“Kama ni kweli Bashite ameongoza watu kufanya uvamizi kwenye kituo cha clouds media kwa jinsi inavyojieleza…Basi atakua mfano wa tumbili aliyemaliza kurukia miti yote sasa ameamua kurukia mwili wa anaemfuga…”

“Na’Anko’akiendelea kushupaza shingo ktk hili huenda yale maandiko yakatimia kabla ya muda tarajiwa…muwe na Jpili Kareem akina ndugu…..”.

Siku ya Ijumaa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia studio za Clouds Media akiwatawa watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kurusha habari kuhusu mwanamke aliyezaa na mchungaji Gwajima.

LEAVE A REPLY