Alichoongea Ruge baada ya kukutanishwa na Makonda leo

0
251

Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameonekana kulilaumu Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika kukutanishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kuyamaliza matatizo yao.

Akiongea na waandishi wa habari leo mbele ya Mhe. Makonda na viongozi wa TEF, Ruge amesema anaona taratibu zilizochukuliwa na jukwaa hilo katika kufanikisha tatizo hilo linaisha halijafuata utaratibu mzuri wakitaalamu.

Ruge amesema kuwa “Mimi sijali kama ataomba radhi au hataomba hiyo haijalishi. Ndio mimi na Makonda ni marafiki sana lakini pia ni mdogo wangu sana na mimi kama kaka yake nilitegemea tungeyamaliza haya kwanza ndio tungekuja hapa,”.

Ruge amesisitiza kuwa wao kama Clouds hawakutoa kauli ya kufungia kuandika habari za Makonda lakini ni TEF walichukuwa maamuzi hayo na wala hawakuviambia vyombo vingine vya habari waingilie ugomvi huo.

LEAVE A REPLY