Alichoongea Neymar baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari

0
229

Mshambuliaji mpya wa klabu ya PSG, Neymar ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari na huku akipewa jezi namba 10 aliyokuwa anavaa kiungo Javie Pastore.

Baada ya kusaini kutambulishwa Neymar amesema kuwa  niilihitaji changamoto mpya katika soka na moyo wangu ulikuwa ukiniambia kwamba PSG ni mahala sahihi kwangu.

Neymar amesema kuwa ni muda sahihi kwake kuondoka Barcelona na kwenda kutafuta changamoto mpya.

Ameongeza kwa kusema kuwa  “Nina furaha sana kuvaa jezi ya Paris Saint German na kubeba jina la taifa langu pamoja na mimi, niko tayari kucheza popote kocha atakapotaka nicheze mimi nataka kucheza soka tu”

Neymar amesema kuwa “Paris Saint German ni klabu ambayo inataka kuja kuwa klabu kubwa duniani na mimi nataka kuwa sehemu ya watu ambao wataandika historia na klabu hii, sikuvutiwa na pesa kuja hapa bali mipango ya klabu hii.

Kwa upande wake mmiliki wa klabu hiyo Nasser Al Khelaifi amesema kwa sasa wanataka kushinda Champions League na sasa wanaenda kupambana kuhakikisha PSG inabeba kombe hilo.

Nasser pia amesisitiza kwamba PSG haikukiuka sheria za Financial Fair Play za FIFA na kusisitiza kwamba UEFA inajua kila kitu kuhusu usajili wa Neymar na hakuna kitu kilichofichwa.

LEAVE A REPLY