Alichoongea Mwakyembe kuhusu Makonda kuvamia Clouds Media

0
281

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa anafahamu kuhusu tukio la uvamizi lililofanyika katika ofisi za Clouds Media Group.

Mwakyembe amesema kuwa yeye kwa sasa hawezi kulizungumzia tukio hilo wala kutoa uamuzi wowote kwa kuwa hajapata ushahidi unaojitegemea.

Ameongeza kuwa bado suala hilo ni la kuchunguzwa zaidi kwani picha inayotolewa ni ya upande mmoja.

Aidha kwa mujibu wa ripoti iliyokuwa imetolewa na kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ilisema kuwa wamesikiliza upande wa mlalamikaji (Clouds Media Group).

Lakini walipokwenda kwa ajili ya kuusikiliza upande wa mlalamikiwa (RC Paul Makonda) hawakufanikiwa kumpata.

Hata hivyo ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ili aifikishe katika mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

LEAVE A REPLY