Alichoongea Mourinho kuhusu kumsajili Gareth Bale

0
103

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa matumaini ya timu yake kumsajili mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale hayapo tena.

Awali Mourinho alisema kuwa angepigania kuweza kumsaini Bale ikiwa Real Madrid wangetaka kumuuza mchezaji huyo raia wa Wales.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez alinukuliwa na gazeti la Uhispania, Marca akisema kwa mabingwa hao wa Uhispania hawana mpango wa kumuuza Bale kipindi hiki.

Bale mwenye umri wa mika 28, alijiunga na Real Madrid kwa kima cha pauni 85 akitokea Tottenham mwaka 2013.

Alitangaza kuama Madrid siku za usoni mwishoni mwa msimu akisema kuwa atakuwa na furaha kusalia na mabingwa hao wa Ulaya mara 12.

Madrid pia wanaripotiwa kuwa na mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Monaco Kylina Mbappe kwa pauni milioni 160.

LEAVE A REPLY