Alichoongea mke wa Roma kwenye siku yake ya kuzaliwa

1
309

Mke wa Mwanamuziki, Roma Mkatoliki, Nancy amesema kuwa alikata tamaa ya kuishi tena na mume wake baada ya kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa studio za Tongwe Records jijini Dar es Salaam.

Nancy alikuwa mmoja kati ya watu walioweza kupambana huku na kule ndani ya siku 4 hizo kutafuta taarifa zilizosaidia kupatikana kwa mume wake huyo ambaye alitekwa pamoja na watu wengine watatu.

Jana wakati anasheherekea siku yake ya kuzaliwa amedai alikata tamaa kama angepata nafasi ya kusherekea siku hiyo muhimu akiwa na mume wake.

Kupitia akaunti yake Instagram ameandika “Ilifika wakati nilikata tamaa na kuamini kuwa sitakuwa na wewe katika sikukuu ya kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ya mwaka huu!! Lakini Mungu Baba Wa Mbinguni akasema no. #MyBirthday2017,”.

Roma na wezake watatu walitekwa na watu wasiojulikana wakiwa Tongwe Record Masaki Jijini Dar es salaam ambapo mpaka sasa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Nancy alipata fursa ya kusherekea siku yake hiyo muhimu akiwa na mume wake ambaye bado anauguza majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa na watu wasiojulikana na baadaye kuachiwa.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY