Alichoongea Makonda kuhusu ujenzi wa barabara Dar

0
100

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka Wajumbe Bodi ya Barabara kuhakikisha fedha zilizotengwa kwaajili ya Ujenzi na Uboreshaji wa Barabara kwa Mwaka 2017- 2018 zinatumika kutengeneza Barabara zenye Ubora.

Makonda amesema hayo wakati wa Kikao cha Bodi ya Barabara ambapo amesema kuwa hataki kuona kwenye Mkoa wake Barabara zinatengenezwa kwa gharama kubwa alafu zinaharibika kwa muda mfupi na kusababisha Kero kubwa kwa Watumiaji wa Barabara.

Amewataka wajumbe wa Bodi hiyo kuhakikisha wanazuia Uharibifu wa Barabara unaofanywa na Magari yanayobeba mizigo mikubwa kupita uwezo wa barabara.

Katika bajeti ya serikali ya mwaka 2017 -2018 imetengwa zaidi ya shilingi Billion 184 kwaajili ya ujenzi wa barabara za mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni ongezeko la zaidi ya 5%.

Makonda ameagiza makampuni yote yanayofanya kazi ya ukamataji wa vyombo vya moto na kufanya kazi hiyo kinyume na mkataba hali inayoleta kero kwa wananchi kuvunja mikataba yao.

Hata hivyo Makonda amewataka watendaji hao kuhakikisha miradi yote iliyokusudiwa kutekelezwa na serikali inamalizika kwa wakati.

Katika kikao hicho kimejumuisha Wabunge, mameya, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalamu wa sekta ya barabara.

LEAVE A REPLY