Alichoongea Faiza Ally kuhusu mapenzi yake kwa Sugu

0
108

Muigizaji wa Bongo Movie, Faiza Ally amedai kuwa bado anampenda Sugu ila hana hisia naye za kimapenzi kutokana na kile kilichotokea kati yao.

Kauli ya muigizaji huyo inakuja siku chache baada ya Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini kutoka jela kwa msamaha wa Rais.

Faiza amesema licha ya yote yaliyotokea kati yao mapenzi yake ya kweli kwa Sugu hayajawahi kuisha.

Amesema kuwa “Hisia na mapenzi ni tofauti, kwa sababu nampenda mapenzi ya kweli hayajawahi kufutika, i will always love him na kumpenda haina maana kuwa nina hisia naye.

Faiza na Sugu wamejaliwa kupata mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Sasha ambaye anaishi na mama yake huyo.

LEAVE A REPLY