Alichokiandika Nandy kuhusu Ruge

0
257

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ametoa ahadi nyingi kwa Ruge kupitia ukurasa wake wa instagram ikiwa ni mara ya kwanza kutoa kauli yake tokea Ruge afariki February 26,2019.

Nandy amesema kuwa ataendelea kumuenzi Marehemu Ruge Mutahaba kwa kufanya kazi kwa juhudi na kufikia malengo waliopanga pamoja na amemalizia kwa kusema kuwa Ruge ni kitu muhimu ambacho hakijawahi kutokea katika maisha yake.

“Kila mtu ana mtu ambaye ameumbwa na MUNGU kwa ajili yake. Na jinsi yakukutana na uyo mtu inaweza ikawa ni ndefu ikawa na matuta mara nyingine inaweza ikakuchosha lakini mwisho wa siku kila kitu kinakuja kuwa sawa.. Wanaweza kutokea watu wachache ambao watakuelewa na pia kuelewa ndoto zako hata kama unazifanya mwenyewe”

“Watakuwa hapo kukupa mrejesho chanya na watakubeba kwenye safari yako kwa moyo wote… Watanzania wanakupenda Umegusa maisha ya watu kwa namna tofauti tofauti Ulizaliwa kuwa kiongozi Ulikuwa na moyo wakutoa.. Ruge ulikuwa rafiki yangu wa karibu sana, ulikuwa kila kitu kwangu Ruge ulielewa ndoto yangu Ruge ulinipa moyo wa kupambana hata kama nilikua nataka ku give up Ruge uliona ndoto yangu na hukuwa na wasiwasi nayo”

“Ulivo pumzika naweza kukuhakikishia nitakufanya ujivunie, nitaendelea kuzi enzi na kuziishi hekima zako Na nitafanya juhudi kufikia malengo tuliyo panga pamoja .Nakupenda sana na nitaendelea kukupenda hata kama haupo nasi.

LEAVE A REPLY