Alichoandika Wema Sepetu kuhusu Diamond Platnumz

0
542

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amempongeza mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa uamuzi wa kusaidia kulipa kodi familia 500 za Kitanzania.

Wema Sepetu ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram “Wanasema unapotoa na Allah pia anakuongeza pale ulipopungukiwa..

Wema ameendelea kwa kuandika Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan basi aende akakuongezeee maradufu. Kutoa kweli ni Moyo na sio utajiri… Maana kama ingekua ni utajiri basi nina imani wangefanya MaDon weeeengi hapa mjini but why YOU.

Ameongeza kwa kuandika kuwa I have always known you to be a sweet & caring person from day 1. Kukumbuka ulipotoka ni moja kati ya sifa ulizonazo na kwenye nyimbo pia ulishawahi kutuambia kuwa , “Na Bata unakulaga wee na Rafiki zako, na kucheza Reggae na maskini wenzako.

Pia ameendelea kuandika ” Hichi unachoenda kufanya ni Zaidi ya bata na Reggae… Mnyonge Mnyongeni Haki yake mpeni.

Unastahili Dua za kheri na Baraka nyingi na nina uhakika tayari unazo na unaenda kuzipata nyingi zaidi na zaidi cause you deserve it.

Mwisho amemalizia kwa kuandika Nimejifkiria sana kupost hii kitu ila kila nikiwaza nisipost, Nafsi inanifurukuta…. Ndo nikasema aaaah jaaamaaanii, nini kujikalfisha nafsi.

 

LEAVE A REPLY