Alichoandika Nuh Mziwanda baada ya Shilole kupigwa

0
110

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amelaani kitendo alichofanyiwa muimbaji na mjasiriamali, Shilole cha kupigwa na kuumizwa vibaya na aliyekuwa mume wake, Uchebe.

 

Nuh ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Shilole, ameandika ujumbe huu “Tuachane na mambo ya Nyuma Ila Nimesikitishwa sana na kitendo Cha kikatili kilichotokea kwako Zuwena ‘inasikitisha sana Kama Baba ambae nna mtoto wa kike pia Nawaza ingetokea kwa mwanangu ningejisikiaje.

 

Nimeishi na wewe takribani miaka minne sikuwahi kugusa mwili wako kwa mabavu ‘yote nilijua una family inakuangalia linaweza kutokea lolote.

Pia amesema kuwa ‘japo kukwazana inatokea sana Tena Mara kwa Mara Ila Kuna Aina ya kumpiga mwanamke na si kwa Aina ya upigaji uliopigwa ‘Nimeumia sana Kama Baba ambaye nna mtoto wa kike pia.

 

Pole sana Zuwena Tunakuombea urudi kwenye hali yako na Hongera Sana Kwa Kusimama kuwakilisha wanawake wanaonyanyaswa na kukaa kimya.

LEAVE A REPLY