Alichoandika Nape baada ya Sugu kutoka jela

0
177

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) amefunguka na kumkaribisha uraiani Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kutoka gerezani.

Nape amefunguka hayo baada ya leo mapema mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kuachiwa kutoka gereza la Ruanda mkoani Mbeya.

Kupitia ukurasa wake mtandao wa kijamii ameandika  “Karibu tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo nilipoanza siasa},”.

Sugu na Katibu wa Chadema Nyanda za Juu kusini walihukumiwa miezi mitano jela katika gereza la Ruanda kwa kosa la kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli.

LEAVE A REPLY