Alichoandika Mnyika baada ya kumtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi

0
179

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika baada ya kwenda kumtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema hakika Mungu ni mkubwa.

Mnyika amesema kuwa tabasamu la Mbunge huyo ni maumivu kwa waliopanga mauaji baada ya kumshambulia kwa risasi.

Kupitia akaunti yake Twitter Mnyika ameandika “Hakika Mwenyezi Mungu ni mkubwa. Tabasamu kama hili ni maumivu kwa waliopanga mauaji. Rais @MagufuliJP aruhusu wachunguzi wa kimataifa waje wafichue ukweli,”.

Mnyika aliongozana na wanachama na viongozi mbali mbali wa Chama cha Demokrasia (Chadema)alifika jana Nairobi hospital kumjulia hali Mbunge huyo.

LEAVE A REPLY