Alichoandika meneja kuhusu Harmonize

0
43

Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize aitwae Beauty Mmali maarufu kama Mjerumani afunguka alivyokutana na msanii huyo mpaka kuanza kufanya kazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mjerumanu ameandika “WAKATI NAKUTANA NA Harmonize KWA MARA YA KWANZA ILIKUA MWAKA 2017 MTWARA, KWANI PROJECT YAKE YA HARMO NIGHT AMBAYO PIA NILISHIRIKI KUIANDAA,NI KATI YA STADIUM EVENTS ZA HARMONIZE AMBAZO ZILIVUNJA RECORD YA MATAMASHA MENGI MAKUBWA NCHINI.

THE WAY ALIVYOKUA ANATOA MIONGOZO NA KWA NAMNA ALOVYOKUA COMMITED NA JAMBO LAKE, NILIMUONA MBALI SANA KWENYE CAREER YAKE, LAKINI SIKUWAI KUDHANI KAMA KUNA SIKU TUNGEFANYA KAZI PAMOJA.

MIAKA 2 BAADAE HARMONIZE ALIONESHA NIA YAKUFANYA KAZI NA MM NA KWASABABU TOKA AWALI NILISHAONA ANA KITU NDANI YAKE, NILIAMINI TUKIUNGANISHA NGUVU TUTAFIKA SEHEMU TUNAYOITAKA NA LEO TUNAMSHUKURU M/MUNGU AMETUJALIA KHERI. YAPO MAMBO MAKUBWA ZAIDI MBELE TUKIJALIWA UHAI INSHALAAH.

HARMONIZE, NILIAMINI KATIKA WEWE SINCE DAY 1 NA AMINI TU CHANGAMOTO NI SEHEMU YA KUJIFUNZA. NAKUPENDA SANA MDOGO WANGU, OUR CEO, NA NITASIMAMIA MAONO YAKO KWA FAIDA YA VIJANA WENGINE NA NCHI YETU PIA. I AM VERY PROUD OF YOU

LEAVE A REPLY