Mama Mobetto aichana familia ya Diamond

0
787

Mama mzazi wa mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobetto, Mama Mobetto amefunguka na kuwataka watu wanaomtukana mtoto wake kuacha tabia hiyo kwani kila binadamu ana mapungufu yake.

Kauli ya mama huyo inakuja kufuatia baadhi ya watu mtandaoni kumtukana mwanamitindo kisa kuzaa na Diamond Platnumz.

Mama huyo amesema kuwa apendi kuona mtoto wake anatukanwa mtandaoni kwani ni kitu kinachomuumiza sana.

Kupitia akaunti yake ya Instagram mama huyo ameandika “Mmenitukania Mwanangu hadi Tumbo la Uzazi limeniuma natamani ningewazaa wawili ili ajifariji kwa mwenzie.

Pia ningeomba familia zote zilizopo Instagram, Mpunguzieni matusi na kumdharilisha Mwanangu, kama kawakosea ninamwombea Msamaha mwezi huu mtukufu . .

Mpeni Amani ili na mimi nifurahie furaha ya Uzazi wangu. Ni mwenyezi Mungu pekee huchagua barabara atakayopitia Mwanaadamu.

Ikumbwe kuwa Hamisa Mobetto amezaa na Diamond mtoto anayejulikana kwa jina la Deylan hivyo mashabiki wa Diamond wamekuwa wakimshambulia Hamisa huku wakimtuhumu yeye ndiyo chanzo cha kuachana kwa Zari na Diamond.

LEAVE A REPLY