Alichoandika Dulla Makabila baada ya wimbo wake kufikisha watazamaji milioni moja

0
27

Baada ya wimbo wa msanii wa singeli Dula Makabila “Nimeghairi kufa” kufikisha watazamaji milioni moja, hatimaye Dulla ameweka ujumbe ake wa shukurani na kujipa sifa kama kawaida kwa mfalme wa singeli yupo mmoja tuu na akifa Taifa limepata hasara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dullamakabila ameandika “Kiukweli Nna Furaha isiyoelezeka Muziki Wa Singeli Nauona Mbali Sana Ni Kiasi Gani Mungu Ametuonesha Mwanga Na Kutupa Heshima Maana Tulipoutoa Mpaka Ulipofika Sio Kitu Kidogo.

Leo Nimeghairi Kufa imepata Views 1m Ndani Ya Mwezi Mmoja Kitu Ambacho Hakijawai Kutokea Tangu Mziki Wa Singeli Uanze Naomba Niweke Sawa hapa ili Wasanii Wenzangu Wa Singeli Wasije Kujiskia Vibaya Sina Maana Kuwa Hakuna Wimbo Wa Singeli Ulowai Kutimiza Milioni Zipo Ila Sio Ndani Ya Mwezi Mmoja.

Asante Mungu Hii Ni Moja Ya Hatua Kubwa Sana Katika Mziki Wangu Sina Budi Kuwashukuru Mashabiki Zangu Na Media Zinazonisapoti Na Ata Zisizonisapoti.

Pia Naheshimu Mchango Wao Katika Singeri Niishukuru Pia Team Yangu Nzima Ya Mirangi Empire Tulioshilikiana Kukamilisha Video Yetu Asanteni Sana Nawapenda Sana.

LEAVE A REPLY