Algeria yapinga matumizi ya kifaransa sekondari

0
132
Utata mkubwa wa matumizi ya lugha ya kifaransa kwenye ufundishaji wa masomo ya sayansi umezuka nchini Algeria huku tahadhari kubwa ikitolewa kwenye kulinda alama ya nchi hiyo kupitia lugha.
Waziri wa elimu wa nchi hiyo, Nouria Benghebrit ndiye aliyetoa mapendekezo ya kutumiwa kwa lugha ya kifaransa ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Vyuo vikuu vya Algeria vinafundisha masomo ya sayansi kwa lugha ya kifaransa lakni shule za chini zinatumia lugha ya kiarabu.
Kumekuwa na angalizo kubwa kuwa wanafunzi wengi wa masomo ya sayansi huanguka kwenye masomo hayo wanapofika mwaka wa kwanza kwenye vyuo vikuu kwasababu ya lugha ya kifaransa hivyo waziri akapendekeza masomo hayo yafundishwa kwa lugha hiyo kuanzia chini.
Lakini wanaopinga pendekezo hilo wanadai kuwa endapo lugha hiyo itapewa nafasi kubwa zaidi itaharibu utambulisho wa taifa hilo lenye wananchi wengi wenye asili ya kiarabu.
Mpango huo ulikuwa na dhumuni la kufundisha kwa lugha ya kifaransa masomo ya hesabu, fizikia na masomo ya asili ya sayansi kwenye shule za sekondari.
Mgogoro huo wa matumizi ya lugha tayari umezua mjadala kuhusu uhusiano wa mataifa ya Ufaransa na Algeria ambayo ni koloni la zamani la nchi hiyo.
Ingawa lugha ya kiarabu ndi lugha ya taifa la Algeria bado vyuo vikuu vya nchi hiyo vinatumia lugha ya kifaransa kwa zaidi ya miaka 50 baada ya nchi hiyo kupata uhuru.

LEAVE A REPLY