Algeria yaanza kuwatimua wahamiaji haramu kutoka Afrika Magharibi

0
122

Nchi ya Algeria imeanza mchakato wa kuwaondoa nchini humo maelfu ya wahamiaji wanaoishi nchini humo bila vibali halali.

Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Algerian League for the Defence of Human Rights (ALDHR) wahamiaji hao wengi wanatokea kwenye nchi za Afrika.

Inakadiriwa kuwa wahamiaji hao wanafikia 1,400 wengi wao wakitokea Afrika Magharibi ambao kwa sasa wameanza kutolewa kwa nguvu kwenye majumba wanayoishi kwenye mji mkuu wa Algeria, Algiers.

Miongoni mwa wahamiaji hao ambao tangu Alhamisi iliyopita wamekuwa wakitolewa kwa nguvu ni wanawake wajawazito na watoto.

Shirika la ALDHR limedai kuwa miongoni mwa wahamiaji waliokuwa wanatolewa kwa nguvu wameumia na kukimbizwa hospitali na wamengine wamepelekwa kwenye vituo vya kusubiria kurudishwa kwao vilivyopo nje ya mji huo.

Hali hiyo inatajwa kusababishwa na ongezeko la wahamiaji hao linalopelekea ugumu wa upatikanaji wa ajira kwa wazawa hali iliyopelekea kutokea kwa mapigano baina ya makundi hayo mawili katika siku za karibuni.

LEAVE A REPLY