Album ya Harmonize yafikisha wasikilizaji milioni 10

0
186

Album ya AFRO EAST ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ambayo ilitoka March 16, mwaka huu imefikisha wasikilizaji Milioni 10 kwenye mtandao wa Audiomack.

Album ina nyimbo 18 na huku nyimbo 8 zikiwa na video kama vile Hujanikomoa, Uno, Mama, Mpaka Kesho, Wife, Never Give Up, Fall In Love na Bed Room.

Hii ni Album ya kwanza tangu aingie kwenye soko la muziki. Idadi hii ya wasikilizaji inaifanya AFRO EAST kuwa album ya kwanza ya msanii wa Tanzania yenye wasikilizaji wengi zaidi kwenye mtandao huo,

Nafasi ya pili inashikiliwa na Diamond Platnumz kupitia album yake ya A Boy From Tanzale yenye wasikilizaji milioni 7.94 iliyotoka mwaka 2018.

Album inayoshika nafasi ya tau kwa kusikilizwa sana ni Albam ya Juma Jux iitwayo The Love Album ambayo hadi sasa ina jumla ya wasikilizaji milioni 7.55.

LEAVE A REPLY