Album ya Darassa yazidi kufanya vizuri

0
81

Album ya Darassa “Slave Becomes A King” imefikisha jumla ya streams Milioni 1 kwenye mtandao wa Boomplay Music ikiwa ni ndani ya wiki mbili tu tangu iachiwe rasmi.

Album hiyo yenye jumla ya mizinga 21 imeendelea kufanya vizuri kwenye mitandao mbali mbali ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni, ikiwemo Apple Music, Deezer, Boomplay na nyinginezo.

Darassa kwenye album hiyo amewashirikisha baadhi ya wasanii kwenye nyimbo hizo huku nyingine akiimba peke yake kwenye album hiyo.

Baadhi ya wasanii walipata shavu na Darassa kuimba kwenye album hiyo ni Alikiba, Nandy, Billnass, Dogo Janja, Maua Sama pamoja na Marioo.

Albam hiyo imetoka mwisho mwaka huu na kupokelewa vizuri na wadau wa muziki ndani nan je ya nchi kutokana na ubora wa nyimbo kwenye album hiyo.

LEAVE A REPLY