Albam ya Radio kutoka leo Uganda

0
75

Kundi la Good lyfe ambalo lilokuwa likiundwa na wasanii, Weasel na Radio, leo linatarajia kutoa album mpya ya msanii Radio, ikiwa umetimia mwaka mmoja tangu afariki dunia.

Msemaji wa msanii huyo amesema album hiyo itaitwa Moses The Great #MTG, na watakuwa wakiachia album zake kwa muda wa miaka 20 mfululizo.

Msemaji huyo amesema album hiyo itakuwa na nyimbo alizoimba mwenyewe Radio kabla hajafariki dunia, ambazo zinaweza kutengeneza album takriban 20.

Radio ambaye jina lake kamili ni Moses Ssekibogo, alikuw amsanii mwenye sauti ya kipekee na kipaji kikubwa cha utunzi wa muziki, alifariki dunia Februari 1, 2018 akiwa hospitali, baada ya kupigwa vibaya na kujeruhiwa kwenye ubongo.

Mpaka sasa, mtu aliyefanya tukio lililopelekea kifo chake bado hajahukumiwa na kesi bado inaendelea.

LEAVE A REPLY