Albam ya Harmonize yaendelea kufanya vizuri

0
203

Album ya Harmonize ya Afro East imesikilizwa mara milioni 7 kwenye mtandao wa usambazaji muziki wa audiomack ndani ya miezi mitatu toka kuachiwa kwa albam hiyo.

Album ya Afro East iliachiwa rasmi mnamo March 14, 2020 huku uzinduzi wake ukiwa umeudhuriwa na viongozi wakuu wa kiserikali, wasanii na wadau mbalimbali wa sanaa ndani na nje ya Tanzania

Kwa idadi hii Album ya Afro East ndiyo Album iliyosikilizwa zaidi kwenye mtandao huo kwa wasanii wa Afrika Mashariki.

Mwanamuziki huyo ameendelea kufanya vizuri kwasasa kutokana na nyimbo zake kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio pamoja na platform mbalimbali za mitandaoni.

LEAVE A REPLY