Albam ya Future ‘High Off Life’ yaweka rekodi Billboard

0
79

Album ya Future ‘High Off Life’ imefanikiwa kuchumpa (debut) na kukamata namba 1 kwenye chart za Billboard 200.

Album hiyo ambayo ni ya Nane kwa rapper Future imefanikiwa kuuza jumla ya nakala (153K) ikiwa ni wiki ya kwanza tangu iachiwe rasmi Mei 15 mwaka huu.

Future ameivunja rekodi yake mwenyewe ya mauzo ambapo High Off Life imeipiku DS2 kwenye mauzo ya wiki ambayo ilitoka mwaka 2015 na kuuza nakala (150K) kwa wiki ya kwanza ikiwemo kuchumpa namba 1 Billboard 200.

Mafanikio ya msanii huyo yamekuja kutokana na kujituma kwake wakati wa uandaaji wa nyimbo zake pamoja na kuwa na mashabiki wengi wanaomsapoti.

LEAVE A REPLY