Albam ya Darassa yafikishwa wasikilizaji milioni 138 mitandaoni

0
36

Album ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Darassa “Slave Become King” imefikisha jumla ya wasikilizaji Milioni 138 kwenye mitandao yote ya kusikilizia muziki duniani ikiwa ni miezi michache tangu iachiwe.

Darassa amewashukuru mashabiki wake kwa kusapoti albam hiyo toka ilivyotoka hadi sasa hivi ambapo inaendelea kufanya vizuri kwenye platform tofauti za muziki.

 

Mwanamuziki huyo ameonesha kuguswa na mafanikio ya albam hiyo ambayo iliachiwa rasmi mwaka jana na kupokelewa vizuri na mashabiki wake.

 

Album hiyo ya “Slave Becomes A King” iliachiwa rasmi Disemba 24, 2020 ikiwa na jumla ya nyimbo 21 alizowashirikisha wasanii tofauti tofauti kama Alikiba, Marioo, Nandy, Abbah, Sho Madjozi na wengineo.

LEAVE A REPLY