Albam ya Country Boy yaweka rekodi

0
53

Albam ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Country Boy iitwayo Yule Boy imekuwa Albam ya kwanza ya Hip Hop Tanzania kusikilizwa zaidi baada ya kusikilizwa mara milioni 1.2 katika mtandao wa Audax.

Ni miezi 8 imepita toka Country aachie Album yake ya Yule Boy ambayo ilipata mapokezi makubwa kwa mashabiki toka ilipotoka mwaka jana.

Sasa kupitia mtandao wa kusambaza muziki Duniani Audio Mack Album hiyo imeweka rekodi nchini Tanzania kwa kuwa Album ya kwanza ya msanii wa HipHop nchini Tanzania kusililizwa zaidi ya mara 1.2Milioni.

Hii ni rekodi mpya kwenye muziki wa Country na muziki wa Hip Hop Tanzania kwa ujumla unaoonekana kutofanya vizuri kwenye Platforms za kusambaza muziki.

Mwanamuziki huyo kwasasa anafanya vizuri kutokana na ubora wa kazi zake anazofanya kwa mashabiki wake mpaka kuweka rekodi.

LEAVE A REPLY