Akothee atoa ya moyoni

0
31

Mwanamuziki wa Kenya Akothee ametoa wosia mzito kwa mashabiki zake kuhusu siku ya kifo chake ambapo amesema anasikitishwa sana na tabia ya misiba ya watu maarufu nchini Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwimbaji huyo ameandika kwamba wasanii misiba yao hufana na husherekewa zaidi kuliko siku za uhai wao.

Hicho kinamsikitisha zaidi na kuamua kusema kwa yeyote ambaye atakuja kwenye mazishi yake aje na chakula kwani hakutakuwa na huduma hiyo.

“Mtu mashuhuri husherekewa zaidi pale anapofariki kuliko akiwa hai, inasikitisha. Acha mtu yoyote asije kwenye msiba wangu na kutarajia huduma yoyote maalum.

Haukuwahi kulipa tiketi ya VVIP wala kutokea kwenye tamasha langu lolote, na pindi nikifa ndio unataka utambulike kama mmoja ya waliohudhuria msiba wa Akothee. Mjinga, Usije.

Nimeielekeza familia yangu kwamba, mwili wangu kama nikifa kabla yao basi upelekwe kutazamwa katika shule ya msingi Rakwaro ili mashabiki zangu waweze kunitazama kwenye eneo lenye nafasi.”

“Hakuna Ex wangu yoyote ambaye atapigania mwili wangu. Tayari hilo nimeliweka sawa. Sitazikwa popote zaidi ya Jakamagambo Rakwaro Kacha. Kama ukitaka kula kwenye msiba wangu basi njoo na chakula chako, usije kuwabughudhi familia yangu kwa sababu hukuwahi kuni-support kwa lolote nilipokuwa hai.”

LEAVE A REPLY