Akon kuanza ujenzi wa mji wake mwakani

0
33

Mwanamuziki wa Marekani, Akon amesema shughuli ya ujenzi wa mji wake nchini Senegal utaanza mwaka ujao.

Akon hakuwatambulisha wawekezaji katika mradi huo lakini amefichua kwamba ufadhili wa theluthi tatu ya dola bilioni sita umepatikana.

Mchoraji ramani wa mji huo mpya, Hussein Bakri amesema idadi ya watu katika mji huo inakadiriwa kufika 300,000.

Akon ambaye jina lake halisi ni Alioune Badara Thiam aliwashirikisha moja kwa moja Wamarekani weusi katika mauzo ya mradi huo.

Alisema kuwa ametangamana na; “Waafrika wenye asili ya Marekani ambao hawaelewi utamaduni wao, Kwa hivyo nilitaka kujenga mji ama kubuni mradi kama huu ambao utawapa motisha ya kuwa na makazi katika nchi yao.

“Unapoamua kuishi Marekani,Ulaya ama mahali kwengine ughaibuni na ungelipendelea kuzuru Afrika, tunataka Senegal iwe kituo chako cha kwanza,” alisema.

LEAVE A REPLY