Akon ashtakiwa na Prodyuza wake kwa utapeli

0
116

Prodyuza wa lebo ya Konvikt Entertainment iliyo chini ya staa, Akon, Leland Clopton amemfungulia mashtaka ya udanganyifu staa huyo na kutaka alipwe fidia ya zaidi ya $1m (TZS 2bn).

Kwenye kesi ya msingi, Leland anadai kuwa staa huyo alikuwa hamuonyeshi malipo yote ya mirabaha ya kazi alizozitengeza chini ya lebo hiyo hivyo kumfanya kudhulumiwa pesa nyingi zilizopatikana kutokamna malipo ya mirabaha.

Clopton anadai kuwa Akon alikuwa akifanya mambo hayo kwa kushirikiana na uongozi wa kampuni hiyo kwa makusudi ili kumkosesha mapato ambayo Akon na wenzake waliyatumia kwa manufaa yao.

Clopton amedai kuwa ingawa amekuwa akilipwa mirabaha kwa kazi alizofanya lakini amedai amekuwa akifichwa malipo ya kazi nyingi alizozalishsa kuliko malipo anayopokea kutokana na kazi hizo.

Sambamba na kumshtaki Akon pia Clopton ameiomba mahakama ivunje mkataba wake na kampuni hiyo.

LEAVE A REPLY