Akaunti ya Youtube ya Beka Flavour yadukuliwa

0
75

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa wadukuzi wa mtandao wamedukuwa akaunti yake ya Youtube na sasa haipo hewani.

Beka ambaye mara ya mwisho aliweka kazi ya Again remix mejikuta akikosa akaunti yake ya mtandao huo kwa siku kadhaa ameamua kuweka wazi hisia zake na kuhoji ni nini amewakosea wanadamu.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika “Kwani mimi nimewakosa nini wanadamu washanihackia Instagram yangu mara mbili nikaanza upya, hii nayotumia sasa ni yatatu.

Pia ameandika Sasa wameona wanihackie YouTube channel yangu , Kweli janamni kweli huu ni uungwana, haya inshallah mungu yupo,” ameandika msanii huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

LEAVE A REPLY