Akanusha kulelewa na wanawake

0
28

Muigizaji wa Bongo Movies, Prince HDV amekana madai ya kulelewa na mwanamke kwa kusema wamama wengi wa mjini wana moyo wa kutoa vitu vyao kuwapa vijana ambao wamebarikiwa vipaji ndiyo maana akipewa hawezi kukataa.

Msanii huyo ambaye amepata umaarufu mkubwa wa kuigiza kama kiben-ten kwenye tamthilia anazocheza amesema kuwa anapata wakati mgumu akiwa mtaani kwake.

“Kuna wakati mwanamke anatokea anakupa mwenyewe hauwezi kukataa ila sio kwamba nalelewa halafu wamama wengi sana wa mjini wana moyo wa kutoa kwa vijana ambao tumebarikiwa vipaji.

Pia ameendelea kusema kuwa wamama wengine wanatusaidia sisi hatuna kitu na wanatusaidia sana kwenye maisha yetu ya kawaida, na kwenye kupewa huwezi kupata bure lazima ujitume”.

LEAVE A REPLY