Akamatwa akifukua kaburi la mlemavu wa ngozi (Albino) aliyezikwa miaka 6 iliyopita

0
371

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia kwa mahojiano zaidi, Jonas John (28) ambaye alikutwa saa 7 usiku akifukua kaburi alilokuwa amezikwa Sister Osisara aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (albinism) miaka 6 iliyopita.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya, Dhahir Kidavashari, amedai kuwa John alikamatwa katika kijiji Mumba kata ya Ilembo, Tarafa ya Isangati Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.

Kamanda Kidavashari amesema kuwa Johna amewataja wenzake wawili ambao hata hivyo walifanikiwa kutoroka baada ya kuwaona Polisi siku ya tukio.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio John na wenzake hao wakiwa na vifaa vya kuchimbia ardhi walikutwa ndani ya uzio wa makaburi hayo huku John akiwa ndani ya kaburi ambalo limeshachimbwa hadi kufikiwa Sanduku ulimowekwa mwili wa marehemu.

Hata hivyo kabla jambo halijatekelezwa polisi walitokea na kumtia nguvuni John abapo wenzake wawili waliokuwa nje ya kaburi walifanikiwa kutorokea kusikojulikana na polisi inaendelea kuwatafuta.

LEAVE A REPLY