Ajibu arejea kuikabili St. Louis ya Shelisheli leo

0
288

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amerejea kwenye kikosi cha timu hiyo na leoakawepo kwenye orodha ya wachezaji watakaikabili St Louis ya Shelisheli.

Yanga itawakaribisha wapinzani wao hao katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ajibu anarejea uwanjani akitokea kupona majeraha ya goti aliyoyapata kwenye Ligi Kuu Bara wakati timu hiyo ilipovaana na Azam FC na Nkomola yeye alipata maumivu ya misuli katika mchezo wa Ruvu Shooting.

 Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu amesema wachezaji hao wameanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzao juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Bavu alisema kurejea kwa wachezaji hao kumeimarisha kikosi chao kutokana na kupunguza idadi ya wachezaji majeruhi waliokuwa wanaiandama timu hiyo.

 Pia amesema kuwa “Niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga kuwa, wachezaji wetu muhimu waliokuwa majeruhi Ajibu na Nkomola wamepona na jana (juzi Jumatano) walianza mazoezi ya pamoja na wenzao.

LEAVE A REPLY