Ajib na Okwi nani kuibuka shujaa leo uwanja wa Uhuru

0
227

Klabu ya Yanga leo inaikaribisha Simba kwenye mechi mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara itakayofanyika leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia saa kumi kamili jioni.

Simba imetua jana kutokea Zanzibar kwa ajili ya mechi hiyo ambapo waliweka kambi katika visiwa hivyo vya karafuu.

Kwa upande wa Yanga wao waliweka kambi mkoani Morogoro kwa ajili ya mechi hiyo ya watani wa jadi ambayo itakayokuwa na msisimko kutokana na timu zote kujiandaa vya kutusha.

Timu hizo zitaingia uwanjani kila mmoja wakiwatazama wachezaji wao hatari kwa upande wa Simba wao watakuwa wakimuangalia sana Emannuel Okwi huku Yanga wakimuangalia Ibrahim Ajib.

Umahiri wa Okwi

Ni mchezaji mwingine ambae yupo kwenye minds za mashabiki,walimu na wachezaji wa timu pinzani kama alivyo Ajib Migomba wa Yanga sc.Ni mchezaji tegemeo katika eneo la mwisho la timu ya Simba.Anamudu kucheza namba zote za pale mbele.Ni hatari zaidi kwenye mipira ya adhabu ndogo (fauls) na ni hatari pia akiacha aka drive mpira katika zone ya timu ya Yanga.Ni mtihani kwa Kevin na mabeki wake,kama alivyo Kichuya pia kwa huyu bwana nidhamu na umakini vinahitajika wakati wa kumkaba.

Umahiri wa Ibrahim Ajib

Ni mchezaji wa kipekee nchini kwa sasa hasa kwenye league yetu.Mchezaji mwenye akili ya mpira na ni “individual brilliant” tena very talented.Ana ball pass,ball control,ball balance na ball possession.Ni hatari zaidi kwa mipira ya adhabu ndogo (fauls).Mabeki wa Simba wanapaswa kuwa makini hasa wakijiepusha kwa kutofanya makosa pale kwenye zone yao.Huyu ndiye mchezaji ambae yupo kwenye minds za washabiki wengi,wachezaji na anae sumbua vilivyo akili za walimu.

LEAVE A REPLY