Ajib awatoa hofu mashabiki wa Yanga

0
293

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema kuwa, matokeo yasiyoridhisha wanayoyapata hivi sasa, ni sehemu ya mchezo, hivyo mashabiki waendelee kuwaunga mkono.

Ajibu ametoa kauli hiyo baada ya  Yanga kutoka suluhu na Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Ajibu alisema matokeo hayo si mazuri, lakini wanaendelea kupambana kuhakikisha wanairudisha furaha ya mashabiki kwa kufanya vizuri kwenye michezo ijayo.

“Mashabiki watulie na waendelee kutuunga mkono ili tuweze kufanya vizuri kwenye mechi zijazo kwa sababu haya matokeo hata sisi hatuyafurahii.

“Matokeo yetu dhidi ya Singida ni sehemu ya mchezo, tulijitahidi sana kuhakikisha tunapata ushindi lakini haikuwa hivyo kwa sababu na wenzetu nao walijipanga, kikubwa ifahamike wazi kwamba, ligi bado mbichi kabisa.

LEAVE A REPLY