Afrika yamlaumu Trump kujitoa makubaliano ya Paris

0
133

Baraza la wazee barani Afrika limelaani kitendo cha Rais wa Marekani, Donald Trump cha kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi yenye lengo la kuikoa dunia na uharibifu wa mazingira.

Mwenyekiti wa baraza hilo, Koffi Annan amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni tisho kubwa kwa kipindi hiki hivyo makubaliano ya Paris ni matokeo ya makubaliano mengi ya ushirikiano na utashi wa kutafuta suluhu ya pamoja ya tatizo la dunia.

Koffi Annan ambaye aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) amesema kuwa hakuna nchi moja inayoweza kuvuruga makubaliano yetu.

Pia amesema kuwa wakati Marekani inajiondoa inadhoofisha na kunyong,onyeza mkataba huu wa kimataifa, lakini bado nchi nyingi zimesimamia msimamo wa pamoja.

Ameongeza kwa kusema kuwa kilicho baki kwa sasa katika mkataba huo wa Paris ni kuongeza juhudi za kutatua matatizao ya mabadiliko ya tabia ya nchi ilikuweza kuikoa dunia na tatizo hilo.

LEAVE A REPLY