Afrika Kusini yaanza kutoa mafunzo ya kazi kwa vijana

0
113
P-492

Serikali na sekta ya biashara nchini Afrika Kusini zimeridhia utekelezaji wa uanzishaji programu ya ajira kwa vijana wenye lengo la kuwachukua vijana milioni moja kwa ajili ya mafunzo kazini kwa malipo katika sekta binafsi kwa kipindi cha miaka 3.

Gharama za programu hiyo zitabebwa na sekta binafsi na itaungwa mkono na serikali kwa mazungumzo maalum ya utoaji wa bakhshishi.

Taarifa za programu hiyo ya ajira kwa vijana imebainika baada ya kufanyika mkutano baina ya Rais Jacob Zuma, Naibu wake Cyril Ramaphosa na watendaji wakuu wa sekta binafsi katika jengo la Umoja Jijini Pretoria.

Katika kufanikisha program hiyo sekta binafsi pia imekusanya kiasi cha randi bilioni 1.5 za Afrika Kusini katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuimarisha biashara ndogo na za kati.

LEAVE A REPLY