Afcon 2017: ‘Hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa viwanja vinasababisha majeruhi’ Caf

0
122

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limekanusha madai kuwa viwanja vinavyotumika nchini Gabon vinawasababishia majeruhi wachezaji.

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Avram Grant amekuwa kocha wa kwanza kutoa shutuma hizo kuwa majeruhi kwa wachezaji wake watano yamesababishwa na ubovu wa viwanja.

Kwenye viwanja vinne vinavyotumika katika mashindano hayo, uwanja wa Port-Gentil umekuwa ukilalamikiwa zaidi lakini hata hivyo ndio utakaotumika kwenye mechi ya robo fainali ya kwanza kati Misri na Morocco na pia umepangwa kutumika kwenye pambano la kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu.

Hata hivyo msemaji wa CAF, Junior Binyam amesema: ‘Haijathibitishwa kisayansi kuwa majeruhi yanatokana na uwanja’

Akizungumza na shirika la utangazaji la BBC, Binyam ameendelea kudai kuwa:

‘Waandishi wa habari wanaleta dhana kuwa majeruhi yanatokana na viwanja lakini hatuwezi kuthibitisha hilo. Hata kwenye ligi ya Uingereza inayoaminiwa kuwa na viwanja vizuri zaidi duniani bado wachezaji wanapata majeruhi’

‘Lakini kila kitu kitaendelea kama kilivyopangwa na tunashukuru kwamba tuliupumzisha uwanja wa Port-Gentil na tukaufanyia marekebisho madogo madogo yaliyotokana na kutumika kwake. Uwanja huu utatumika kwenye mechi ya robo fainali na kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu kama ilivyopangwa’

LEAVE A REPLY