Above In a Minute ya Navy Kenzo yaweka rekodi mpya Bongo

0
292

Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na mastaa wawili wapenzi, Nahreel na Aika limeweka historia ya kuwa kundi la kwanza kutoka Tanznaia ambalo albamu yake inauzwa na mitandao mingi zaidi.

Kundi hilo ambalo liliachia albamu ya ABOVE IN A MINUTE a.k.a AIM kwa njia ya CD hivi karibuni limetangaza kupatikana kwa albamu hiyo kwa njia ya mtandao kupitia mitandao ya iTunes, Spotify, Tidal, Akazoo na Boom Player.

Wiki chache zilizopita staa wa kundi hilo, Aika alinukuliwa na vyombo vya habari akilalamika kusambazwa kwa albamu hiyo mitandaoni kwa njia zisizo halali.

Hata hivyo wakali hao wa Navy Kenzo walisisitiza uwa wataiachia albamu hiyo mtandaoni na kuwaachia mashabiki wajipime uungwana wao endapo wataamua kuipata bure kwa njia zisizo halali au wataamua kusapoti jitihada za wasanii hao kwa kununua kazi halisi.

Albamu hiyo ina nyimbo mbalimbali za collabo ambazo mastaa wa Bongo na wengine kutoka nje wameshirikishwa.

LEAVE A REPLY